The web Browser you are currently using is unsupported, and some features of this site may not work as intended. Please update to a modern browser such as Chrome, Firefox or Edge to experience all features Michigan.gov has to offer.
Language services - Kiswahili (Swahili)
Translated resources
Fasil ya kivinjari (chagua kichupo) (Browser translation (Choose tab))
-
Kanusho (Disclaimer)
-
Safari (Safari)
-
Google Chrome (Google Chrome)
-
Microsoft Edge (Microsoft Edge)
Idara ya Jimbo la Michigan haiwajibiki kisheria kwa uharibifu au madhara yoyote yanayoweza kusababishwa na matumizi ya tafsiri zozote zinazotolewa na programu au kivinjari cha wahusika wengine. Matumizi ya huduma yoyote ya muhusika mwingine itakuwa ni hiari ya mtumiaji pekee. Taarifa zinazohusiana na huduma za wahusika wengine hutolewa kama zinafaa pekee.
Safari hutoa tafsiri katika Kiarabu, Kichina (Kilichorahisishwa), Kifaransa, Kijerumani, Kiitaliano, Kijapani, Kikorea, Kireno, Kirusi, na Kihispania.
Eneo-kazi (desktop)
1. Fungua kivinjari cha Safari na uchague Vie, kisha Tafsiri kwenye menyu kunjuzi.
2. Weka kivinjari chako katika lugha inayopendelewa, ambayo si Kiingereza.
3. Nenda kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri.
4. Kitufe cha kutafsiri kitaonekana upande wa kulia wa upau wa anwani. Huenda tafsiri zisipatikane kwa kurasa zote.
5. Chagua kitufe cha kutafsiri na lugha unayoipendelea.
iPhone au iPad (iPhone or iPad)
1. Fungua kivinjari cha Safari kwenye kifaa chako cha mkononi na uende kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri.
2. Chagua alama ya "aA" iliyo karibu na upau wa anwani ili kuona machaguo ya tovuti. Kwenye menyu kunjuzi, chagua Tafsiri kuwa na lugha unayopendelea.
3. Chagua Washa Tafsiri ikiwa menyu ibukizi itaonekana. Kumbuka kwamba utaombwa kuwasha tafsiri mara moja pekee.
Vifaa vya Apple vyenye mifumo endeshi ya zamani zaidi ya IOS 14.0, haitajumuisha kipengele hiki. Pakua programu ya Google Translate au programu ya Microsoft Translator kwenye kifaa chako ili kupata tafsiri.
Eneo-kazi (desktop)
1. Fungua kivinjari cha Chrome na uende kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri. Menyu ibukizi ya Tafsiri ya Google inaweza kuonekana chini ya upau wa anwani.
2. Chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu ili kutafsiri ukurasa huo.
3. Ikiwa menyu ya kutafsiri haionekani, chagua kitufe cha Google Translate kilicho upande wa kulia wa upau wa anwani. Chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu ili kutafsiri ukurasa huo.
4. Ili kupata lugha nyingi zaidi kwa ajili ya tafsiri, chagua kitufe cha Google Translate kilicho upande wa kulia wa upau wa anwani, kisha chagua alama ya menyu ya kitendo.
5. Kwenye menyu kunjuzi, teua Chagua Lugha Nyingine na uchague lugha unayopendelea kwenye menyu kunjuzi.
Simu au kishikwambi cha Android (Android phone or tablet)
1. Fungua kivinjari cha Chrome kwenye kifaa chako cha mkononi na uende kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri.
2. Menyu ya Tafsiri ya Google inaweza kuonekana chini ya skrini.
3. Chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu ili kutafsiri ukurasa huo.
4. Ili kupata lugha nyingi zaidi za kutafsiri, chagua alama ya menyu ya vitendo na uchague Lugha Zaidi kisha chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu kunjuzi.
- Unapofungua kivinjari cha Microsoft Edge, chagua nukta tatu kwenye kona ya juu kulia ya kivinjari chako kisha, chagua Mipangilio kwenye orodha kunjuzi.
- Chagua Lugha, upande wa kushoto wa dirisha la kivinjari chako na uweke lugha unayoipendelea kwa kuchagua Ongeza lugha na kufuata vidokezo.
- Ukitembelea ukurasa ambao haujatafsiriwa katika lugha unayoipendelea, menyu ibukizi ya tafsiri inaweza kuonekana kwenye upau wa anwani.
- Fuata vidokezo ili kuchagua lugha unayoipendelea na uchague Tafsiri ili kutafsiri ukurasa huo.
Miamala na huduma za Katibu wa Jimbo (Secretary of State transactions and services)
-
Huduma za mkalimani (Interpreter services)
liHuduma za mkalimani (Interpreter services)
Iwapo unahitaji kufanya mtihani, kuhudhuria kikao cha kurejeshewa leseni, au kukamilisha uchunguzi mpya wa leseni, lazima utumie mkalimani ambaye ameidhinishwa na Idara ya Jimbo la Michigan kabla ya miadi yako iliyopangwa.
Unaweza kumuomba mtu yeyote atafsiri kwa niaba yako kwa huduma zingine zote za Katibu wa Jimbo na ziara za ofisi.
Wakalimani wa kujitolea wa kudumu (Permanent volunteer interpreters)Taarifa kuhusu wakalimani wa kudumu walioidhinishwa inapatikana kwa kupiga simu 888-SOS-MICH (888-767-6424) au kwa kutembelea ofisi ya Katibu wa Jimbo.
Wakalimani walio kwenye orodha hii wameidhinishwa kutoa huduma katika afisi mahususi za Katibu wa Jimbo na hawaruhusiwi kutoza ada.
Ili kuomba nakala ya orodha ya wakalimani walioidhinishwa kabla, tembelea ofisi ya Katibu wa Jimbo au tuma barua pepe kwenda MDOS-Access@Michigan.gov.
Watu wa kujitolea mara moja (One-time volunteers)Iwapo ungependa mtu fulani akutafsirie kwa niaba yako kwa ajili ya mtihani, usikilizaji wa shauri, au kuchunguzwa upya, atapaswa kutuma ombi la kufanya kazi kama mkalimani wa mara moja. Mkalimani wako wa mara moja lazima aidhinishwe na Idara kabla ya ziara yako iliyopangwa na anaweza tu kutoa huduma ya ukalimani kwa ajili ya mtihani, usikilizaji wa shauri lako, au kuchunguzwa upya.
Ili kutuma maombi ya kuwa mkalimani wa mara moja, mtu lazima:
- Ajaze na kusaini Maombi ya Kutoa Huduma za Ukalimani wa Kujitolea, huku akichagua kwamba atafanya kazi kama mkalimani wa mara moja.
- Atoe picha au nakala ya leseni ya udereva au kitambulisho chake halali ambacho muda wake haujaishatembelea
Tuma kwa njia ya barua, faksi au barua pepe hati zote zinazotakiwa kwenda:
Michigan Department of State
Enforcement Division
P.O. Box 30708
Lansing, MI 48909
Faksi: 517-335-3241
Barua pepe: SOS-OIS@Michigan.gov
Mara baada ya Idara kupitia maombi, wafanyakazi watawasiliana na mwombaji ili kumjulisha pindi atakapoidhinishwa kutoa huduma za mkalimani wa mara moja. -
Mitihani ya maarifa ya iliyotafsiriwa (Translated driver knowledge exams)
Ofisi zote za Katibu wa Jimbo hutoa majaribio yaliyotafsiriwa kwa mitihani ya maarifa ya udereva katika lugha zifuatazo:
- iingereza
- Kialbania
- Kiarabu
- Kichini
- Kifaransa
- Kigiriki
- Kihindi
- Kiitaliano
- Kijapani
- Kikorea
- Kipolandi
- Kireno
- Kirusi
- Kihispania
- Kiukreni
- Kivietinamu
Mitihani ya uidhinishaji wa dereva, baiskeli moto, pikipiki, na burudani (Double R) pia hutolewa katika lugha zifuatazo katika ofisi za Katibu wa Jimbo:- Kiingereza
- Kihispania
- Kiarabu
Taarifa za Leseni na Kitambulisho
-
Kamilisha miamala mtandaoni (Complete transactions online)
Miamala mingi sasa inaweza kukamilishwa mtandaoni, ikiwemo uhuishaji wa bamba la gari, leseni ya udereva au uhuishaji wa kitambulisho cha jimbo, na ombi la nakala mbili za hati miliki. Kwa kutumia kipengele cha kutafsiri kiotomatiki kwenye kivinjari chako, unaweza kuipata tovuti yetu na kukamilisha miamala ya mtandaoni kwa lugha unayoipendelea. Tembelea ukurasa uliotangulia ili kuona maelekezo ya tafsiri ya kiotomatiki ya tovuti ya Idara ya Jimbo.
-
Vituo vya kujihudumia (Self-Service stations)
Tembelea kituo cha kujihudumia ili kuhuisha usajili wa gari lako, nembo na bamba la gari au kuhuisha leseni au kitambulisho chako, ikiwa picha mpya haihitajiki. Vituo vyote 160 vya kujihudumia vya Katibu wa Jimbo vinatoa huduma iliyotafsiriwa katika lugha zifuatazo:
- Kiarabu
- Kibengali
- Kiingereza
- Kifaransa
- Kimandarini
- Kipashto
- Kihispania
- Kivietinamu
Ada ya huduma ya $3.95 itatozwa kwa kila bidhaa itakayotumika kwenye kituo cha kujihudumia.
-
Tembelea ofisi ya Katibu wa Jimbo (Visit a Secretary of State office)
Miamala mingi ya Katibu wa Jimbo inaweza kukamilishwa mtandaoni au kwa barua. Miamala mingi ya leseni ya udereva na vitambulisho na miamala mingi ya kuhuisha nembo ya gari inaweza kukamilishwa kwenye kituo cha kujihudumia. Iwapo utahitajika kutembelea afisi ya Katibu wa Jimbo, unahimizwa sana kupanga ziara ya ofisi. Ziara zinaweza kupangwa hadi miezi sita kabla au siku inayofuata. Maelfu ya ziara za ofisini hutolewa kila siku ya kazi (Jumatatu-Ijumaa) saa 2 asubuhi na mchana kwa siku inayofuata ya kazi.
Pia unaweza kwenda kwenye ofisi yoyote na utahudumiwa papo hapo, kama kuna nafasi, au watakusaidia kupanga ziara ya ufuatiliaji kwa siku hiyo hiyo au siku inayofuata.
Ili kupanga ziara mtandaoni katika lugha unayoipendelea, hakikisha kuwa unatumia kivinjari kinachotoa kipengele cha kutafsiri kiotomatiki. Au, panga ziara ya ofisini kwa kupiga simu 888-SOS-MICH (888-767-6424).
Panga ziara ya ofisiniVinjari tafsiri - Huduma za lugha
Taarifa za uchaguzi na mpiga kura (Elections and Voter information)
-
Usajili wa mpiga kura (Voter registration)
Unaweza kujiandikisha ili kupiga kura katika jimbo la Michigan iwapo wewe ni: (You can register to vote in Michigan if you are:)
- Raia wa Marekani
- Una umri wa angalau miaka 17.5
- Kwa sasa hutumikii kifungo jela au magereza
- Mkazi wa Michigan
Angalia hali yako ya usajili (Check your registration status)
Kwa kutumia kivinjari chenye kipengele cha kutafsiri kiotomatiki, unaweza kuangalia hali yako ya usajili wa mpigakura kwenye Michigan.gov/Vote.
Jinsi ya kujiandikisha (How to register)
Unaweza kujiandikisha ili kupiga kura mtandaoni (ukiwa na leseni na namba ya kitambulisho cha ya Michigan) au kwa barua hadi wiki 2 kabla ya Siku ya Uchaguzi. Pia unaweza kujiandikisha moja kwa moja katika ofisi ya karani wa eneo lako wakati wowote kabla na hadi saa 2 usiku katika Siku ya Uchaguzi.
Huna haja ya leseni au kitambulisho cha Michigan ili kujiandikisha kupiga kura kwa barua au katika ofisi ya karani wa eneo lako na badala yake unaweza kutoa tarakimu nne za mwisho za namba yako ya Hifadhi ya Jamii.
Tafadhali kumbuka kwamba ndani ya siku 14 baada ya uchaguzi, ni lazima ujiandikishe moja kwa moja katika ofisi ya karani wako ukiwa na uthibitisho wa ukaazi wako.
Jiandikishe mtandaoni: (Register online) Tumia kivinjari chenye kipengele cha kutafsiri kiotomatiki ili kupata usajili wa mpigakura mtandaoni katika lugha unayoipendelea kwenye Michigan.gov/Vote
Unaweza kujiandikisha mtandaoni ikiwa:
- Una Kitambulisho au Leseni ya Udereva ya Michigan
- Unazijua tarakimu 4 za mwisho za namba yako ya hifadhi ya jamii
- Una umri wa angalau miaka 17.5
- Hauko ndani ya siku 14 za Siku ya Uchaguzi
Ukijiandikisha mtandaoni ndani ya siku 14 baada ya uchaguzi au siku ya uchaguzi, hutatimiza vigezo vya kupiga kura katika uchaguzi huo. Uandikishaji wa mtandaoni hauruhusiwi ndani ya siku 10 baada ya kuhuisha kitambulisho au leseni yako ya Udereva.
Vinjari tafsiri - Huduma za lugha
Jiandikishe kwa kutumia Fomu ya Usajili Inayoweza Kuchapishwa: (Register Using a Printable Registration Form) Unaweza kujiandikisha kupiga kura kwa kutumia fomu ya kujiandikisha kupiga kura iliyotafsiriwa, na inayoweza kuchapishwa. Unaweza kujiandikisha kwa kutumia fomu ya kujiandikisha iliyochapishwa ikiwa:
- Una Kitambulisho au Leseni ya halali ya Udereva ya Michigan au una tarakimu 4 za mwisho za namba yako ya hifadhi ya jamii (kimoja tu kinahitajika).
- Una umri wa angalau miaka 17.5
- Hauko ndani ya siku 14 za Siku ya Uchaguzi
Fomu ya Kujiandikisha Kupiga Kura Inayoweza Kuchapishwa
Jiandikishe kwenye Kioski cha Kituo cha Kujihudumia: Vituo vya Kujihudumia vinashughulikia usajili wa wapigakura katika lugha nyingine ambazo si Kiingereza. Tazama sehemu ya Kituo cha Kujihudumia katika ukurasa huu wa tovuti kwa taarifa zaidi.
Jiandikishe moja kwa moja kwenye ofisi ya karani: (Register in-person at your clerk’s office) Unaweza kutembelea ofisi ya karani wa eneo lako ili kujisajili moja kwa moja kupiga kura. Ndani ya siku 14 za Uchaguzi, lazima ujiandikishe moja kwa moja katika ofisi ya karani wa eneo lako na lazima uwasilishe uthibitisho wa makazi. Uthibitisho wa makazi ni hati rasmi inayotaja jina lako kamili na anwani yako ya sasa, na unaweza kujumuisha taarifa ya benki, leseni ya Udereva au Kitambulisho halali cha MI, mkataba wa upangaji, au bili ya huduma za jamii.
Mtafute karani wa eneo lakokupiga kura kwenye uchaguzi (Voting in an election)
Kupiga kura kwenye uchaguzi, lazima uwe:
- Mpigakura wa Michigan uliyejiandikisha
- Una umri wa angalau miaka 18
- Kwa sasa hutumikii kifungo jela au magereza
- Mkazi wa jiji, kitongoji, au kijiji kile kile cha Michigan kwa angalau siku 30 kabla ya uchaguzi
Una haki ya kupiga kura ya siri. Ukiwa kama mpiga kura wa Michigan, unaweza kuomba na kupiga kura kwa kutohudhuria katika uchaguzi wowote bila kutoa sababu.
-
Upigaji kura wa kutohudhuria (kutoka nyumbani, kwa barua, au mapema katika ofisi ya karani wako) (Absentee Voting)
Kuomba upigaji kura wa kutohudhuria (Applying for an absentee ballot)
Kila mpiga kura aliyejiandikisha Michigan anaweza kupiga kura kwa kutumia kura ya mpiga kura ambaye hayupo (AV). Ili kuomba kura ya AV, ni lazima ujaze na uwasilishe Ombi la Kura ya Mpiga Kura ambaye hayupo.
Machaguo ya kukamilisha ombi la kura ya mpiga kura ambaye hayupo:
- Kamilisha na utume ombi mtandaoni kwa kutumia kivinjari chenye kipengele cha kutafsiri kiotomatiki.
- Mpige simu karani wa jiji au mji wako na uombe kutumiwa ombi lililochapishwa kwa njia ya barua.
- Pakua ombi linaloweza kuchapishwa, lililotafsiriwa ambalo utalirudisha kwa njia ya barua au moja kwa moja kwa karani wa eneo au mji wako.
- Moja kwa moja kwenye ofisi ya karani wa eneo lako iliyoteuliwa.
Maombi yaliyokamilishwa lazima yapokewe na karani uliyemchagua kwa njia ya barua, barua pepe au uyapeleke mwenyewe kabla ya saa 11:00 jioni Ijumaa kabla ya Siku ya Uchaguzi.
Kukamilisha na Kurejesha Kura yako ya Mpiga Kura ambaye hayupo (Completing and Returning Your Absent Voter Ballot)
Fuata maelekezo kwenye fomu ya maombi ya mtu ambaye hayupo, na uchague ni uchaguzi gani ungependa kupokea kura ya kutohudhuria. Wapiga kura wanaweza pia kuchagua kisanduku ili kuomba kura za watu wasiohudhuria watumiwe kwa kila uchaguzi unaoendelea.
Baada ya kutuma maombi yaliyokamilika, kura itatumwa kwenda kwenye anwani yako. Unaweza pia kutembelea ofisi ya karani wa eneo lako ndani ya siku 45 za siku ya uchaguzi ili kuomba na kuwasilisha kura ya kutohudhuria. Soma maelekezo ya kura ya mtu ambaye hayupo kwa makini ili kukamilisha kura yako. Rudisha kura yako ya mtu ambaye hayupo pamoja na bahasha iliyotiwa hahihi kabla ya saa 2 usiku katika Siku ya Uchaguzi.
Machaguo ya kurudisha kura iliyokamilika bila kuwepo kwa wapigakura:
- Wasilisha kwa mkono kura yako iliyokamilika kwa karani mteule wa eneo lako ana kwa ana.
- Tuma kura yako iliyokamilika kwa karani mteule wa eneo lako (haipendekezwi ndani ya wiki 2 za Siku ya Uchaguzi).
- Tumia eneo la sanduku la barua la karani aliyeteuliwa.
Ombi la kura ya AV la mtandaoni
-
Kupiga kura siku ya kupiga kura (Voting on election day)
Kupiga kura katika kituo cha kupigia kura (Voting at your polling place)
Unaweza kupiga kura moja kwa moja katika Siku ya Uchaguzi kwenye eneo lako ulilochagua kupigia kura. Katika kila uchaguzi, upigaji kura hufunguliwa kati ya saa 1 asubuhi na saa 2 usiku. Ikiwa uko katika mstari wa kupiga kura saa 2 usiku wakati upigaji kura unafungwa, bado unaweza kupiga kura na unahimizwa kusalia kwenye foleni ili kupokea kura yako.
Ukiwa kama mpiga kura aliyesajiliwa Michigan, una haki ya kuja na mkalimani kwenye uchaguzi. Unaweza kumuomba mtu yeyote kufanya kazi kama mkalimani, isipokuwa kama ni mtu ambaye anaweza kushawishi kura yako. Mkalimani wako hawezi kuwa:
- Mwajiri wako
- Wakala wa mwajiri wako
- Afisa au wakala wa chama chako cha wafanyakazi
Kujua kituo chako cha kupigia kura, tembelea Michigan.gov/Vote.
-
Fahamu kile kilicho kwenye kura (Learn what’s on the ballot)
Kwa kutumia kivinjari chenye kipengele cha kutafsiri kiotomatiki, unaweza kuangalia hali yako ya usajili wa mpigakura kwenye Michigan.gov/Vote.
Vinjari tafsiri - Huduma za lugha
-
Haki zako za kupiga kura (Your voting rights)
Matumizi ya lugha (Language Access)
Wakazi wa Michigan wana haki ya kuja na mkalimani asiye Mwingereza kwenye uchaguzi kwa ajili ya msaada wa kupiga kura. Mkalimani wako hawezi kuathiri kura yako, hawezi kuwa mwajiri wako, wakala wa mwajiri wako, au afisa au wakala wa chama chako cha wafanyakazi.
Hakuna masharti ya kitambulisho chenye picha (No photo identification requirement)
Ikiwa huna kitambulisho chenye picha, bado unaweza kupiga kura.
Upigaji kura wa kutohudhuria bila sababu (No-reason absentee voting)
Kila mpigakura aliyejiandikisha katika jimbo la Michigan ana haki ya kutumia kura ya mpigakura ambaye hayupo kupiga kura nyumbani, kupiga kura mapema au kupiga kura kwa njia ya barua.
Uandikishaji wa wapigakura siku hiyo hiyo (Same-day voter registration)
Wakazi wa Michigan wanaostahiki wanaweza kujiandikisha kupiga kura Siku ya Uchaguzi kwa kutembelea ofisi ya karani aliyeteuliwa na kutoa uthibitisho wa makazi.
Raia wanaorudi nyumbani (Returning Citizens)
Wakazi wa Michigan ambao kwa sasa hawatumikii kifungo jela au magereza wana haki ya kujiandikisha kupiga kura na kupiga kura.
Ufikivu wa wapiga kura (Voter accessibility)
Wapiga kura wa Michigan wana haki ya kuyafikia maeneo ya kupigia kura na kuvitumia Vituo vya Msaada wa Wapiga Kura (VAT) ili kupata usaidizi wa kupiga kura. VAT ni vifaa vya kuwekea kwenye kura vyenye vitu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kusikia, kuona, mwili na ulemavu mwingine. Wapiga kura wana haki ya kupiga kura kwa uhuru na faragha bila msaada wa kutumia VAT, na wakaguzi wa uchaguzi wa kituoni (wasimamizi wa uchaguzi) wanapatikana ili kutoa msaada au kutoa maelekezo wanapoombwa.
-
Mamlaka za tafsiri za uchaguzi za serikali ya mtaa (Local election translation mandates)
Jamii zifuatazo zinatakiwa kisheria au kanuni kutoa nyenzo za uchaguzi zilizotafsiriwa katika lugha mahususi:
- Jiji la Fennville: Kihispania*
- Mji wa Colfax: Kihispania*
- Mji wa Clyde: Kihispania*
- Jiji la Dearborn: Kiarabu
- Jiji la Hamtramck: Kiarabu
- Jiji la Hamtramck: Kibengali*
*Huonyesha sharti la kisheria la kutoa kura zilizotafsiriwa kulingana na Sheria ya Haki za Kupiga Kura
Ukiwa kama mpiga kura aliyesajiliwa Michigan, una haki ya kuja na mkalimani kwenye uchaguzi. Angalia “Haki zako za kupiga kura” zilizo hapo juu kwa taarifa zaidi.
-
Simu ya dharura ya ulinzi wa uchaguzi (Election protection hotline)
Ukikumbana na matatizo yoyote wakati wa kupiga kura kabla au kabla ya Siku ya Uchaguzi, wasiliana na Namba ya Simu ya Ulinzi wa Uchaguzi kwa msaada:
- Kiingereza: 866-OUR-VOTE (866-687-8683)
- Kihispania: 888-VE-Y-VOTA (888-839-8682)
- Kiarabu: 844-YALLA-US (844-925-5287)
- Kibengali, Kikantoni, Kihindi, Kikorea, Kimandarini, Kitagalog, Kiurdu, na Kivietinamu: 888-API-VOTE (888-274-8683)
Fomu na machapisho (Forms and publications)
Tafuta nyenzo na zana za uchaguzi zilizotafsiriwa kwa kutumia menyu ya Fomu na Machapisho. Chagua lugha unayoipendelea kwa kutumia Lugha ili kuchuja kutazama hati zote zilizotafsiriwa.