The web Browser you are currently using is unsupported, and some features of this site may not work as intended. Please update to a modern browser such as Chrome, Firefox or Edge to experience all features Michigan.gov has to offer.
Kiswahili
Kitengo cha Kuzuia na Kudhibiti Saratani cha MDHHS kinalenga kutoa nyenzo kwa wote. Tunafurahi kutoa huduma za tafsiri na ukalimani ili kukusaidia kukuunganisha na nyenzo na huduma unaohitaji.
Huduma za Tafsiri na Ukalimani
Ikiwa wewe au mtu unayemjua anahitaji usaidizi wa lugha, tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe, katika lugha yako, kwenye MDHHS-CPCS-LANG@michigan.gov. Tutawasiliana nawe ndani ya saa 48 (siku 2 za kazi). Iwapo ni dharura ya matibabu, tafadhali piga simu 9-1-1.
Vidokezo kwa Watu Wenye Uwezo Mdogo wa Kuzungumza Kiingereza
- Ikiwa unahitaji msaada wa lugha, omba upatiwe mkalimani, ni haki yako! Wakalimani wa matibabu wenye sifa wamepatiwa mafunzo kutafsiri taarifa za afya kwa ufasaha. Pia wamefunzwa mahitaji yote ya Faragha ya Taarifa za Afya (Sheria za HIPAA) ili kuweka maelezo yako kuwa ya faragha.
- Huduma za ukalimani zenye vigezo zinapatikana kwa ajili yako bila malipo. Hupaswi kumuomba mwanafamilia au rafiki akupatie huduma ya ukalimani. Huenda wasiwe na ujuzi sahihi wa kutoa huduma hizi.
- Unapotembelea ofisi na kliniki za afya, onyesha Kadi ya Ninazungumza kwa mfanyakazi ambaye anaweza kukutafutia mkalimani.
- Omba mkalimani unapomwona daktari au mtaalam wako wa huduma za msingi.
- Omba huduma za ukalimani na tafsiri unapopata huduma zingine, kama vile vipimo vya maabara, uchunguzi wa utambuzi, tiba ya viungo, au ushauri nasaha.
- Kama unafahamu kwamba utahitaji mkalimani, mwambie daktari wako au mfanyakazi wa ofisi hiyo haraka kadri uwezavyo.
- Mwombe daktari, mpango wako wa afya, na duka lako la dawa lijumuishe ombi na mahitaji yako ya lugha ili kupata mkalimani katika taarifa zako za matibabu.
- Wasiliana na Ofisi ya Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani ya Haki za Kiraia (OCR) ikiwa unaamini kuwa haki zako za kupata huduma za lugha zimekiukwa.
Ikiwa Wewe ni Kiziwi au Unasikia kwa Shida
Una haki ya kupata mkalimani wa lugha ya ishara ikiwa unahitaji. Haki hii inalindwa na Sheria ya Wamarekani wenye Ulemavu. Kitengo cha Saratani cha MDHHS hutoa huduma za ukalimani kwa watu ambao ni viziwi au wenye tatizo la kusikia (DHOH). Ili kupanga mkalimani wa Lugha ya Ishara ya Marekani (ASL), tafadhali tuma barua pepe kwenda MDHHS-CPCS-LANG@michigan.gov.